EN SW
⚡

Badilisha Picha za WebP, JPG na PNG

Geuza picha za WebP kwenda JPG/PNG au geuza picha za kawaida kuwa WebP ili kupunguza ukubwa na kuongeza kasi ya tovuti yako papo hapo.

Mifumo Rasmi ya Serikali na Taasisi Inayounga Mkono Huduma Hii:
Picha Zilizokamilika Tayari kwa Kupakuliwa: 0

Mwongozo wa Kitaalamu: Kwa nini Ugeuze WebP kuwa JPG au PNG?

Ingawa muundo wa WebP ni mzuri kwa spidi ya mitandao ya kijamii na tovuti, mifumo mingi ya serikali na ya kiofisi kama vile Ajira Portal (Utumishi), NIDA, au mifumo ya vyuo vikuu inahitaji picha ziwe katika mfumo maalum wa JPEG au PNG. GridPhoto inakusaidia kubadilisha miundo hii kwa usalama na kwa urahisi mkubwa ndani ya kifaa chako.

Usalama na Faragha ni 100%: Picha zako haziondoki kwenye kifaa chako. Kazi yote inafanyika ndani ya kivinjari chako kwa kutumia HTML5 Canvas. Mfumo unasimamiwa na Kizumari Technologies | Mhandisi Suleiman Nassoro Ally.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

❓ Kwa nini picha yangu ya WebP haikubaliwi kwenye mifumo rasmi ya serikali? Mifumo mingi ya maombi na usajili inahitaji miundo ya kawaida kama JPG au PNG kutokana na mifumo yao ya zamani. Kubadili WebP kwenda JPG kunasuluhisha hili haraka.
❓ Naweza kubadilisha picha nyingi kwa wakati mmoja? Ndio! Unaweza kuchagua picha nyingi kwa pamoja, ukachagua format unayotaka, na ukazipakua moja kwa moja.
❓ Je, picha zangu zinatumwa kwenye server za nje wakati wa kubadilishwa? Hapana! Kila kitu kinafanyika ndani ya kivinjari chako (browser) kwa usiri kamili na kasi kubwa.