Lang: SW | EN
📲

QR Code Generator Studio Pro

Tengeneza QR Code za kiofisi, biashara, Wi-Fi, na mawasiliano zenye nembo (logo) na rangi zako. Mfumo ni salama 100% kwani kila kitu kinatengenezwa ndani ya kifaa chako.


🎨 Muonekano & Rangi (Custom Styling):
ONYESHO LA QR CODE (PREVIEW)

Kwa Nini Unahitaji QR Code zenye Nembo na Rangi za Biashara Yako?

Siku hizi, Wateja na wageni wa maofisini hawataki kuandika manenosiri marefu ya Wi-Fi au kuandika namba za simu kwa mkono. Ukiseti QR Code ya Wi-Fi au ya vCard kwenye kadi ya biashara (Business Card), meza ya risiti au mabango, mtu anai-scan kwa kamera ya simu na kupata huduma papo hapo. Zana hii ya GridPhoto inakusaidia kuunda QR Code za kitalaamu zenye nembo yako katikati.

🔒 Utunzaji wa Faragha (Client-Side HTML5 Canvas) Manenosiri yako ya Wi-Fi, namba za simu binafsi, na maelezo ya mawasiliano hayapakiwi wala kuhifadhiwa kwenye server yoyote. Mfumo wetu unatumia JavaScript Canvas kutoa picha ya QR Code moja kwa moja ndani ya kivinjari chako.

Zana Hii Inatunzwa na Kuendeshwa na Kizumari Technologies | Mhandisi Suleiman Nassoro Ally

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)

❓ Je, nikieka logo katikati ya QR Code bado itaweza kusomeka? Ndiyo! Injini yetu inatumia uwezo wa juu wa Error Correction (Level H), ambao unaruhusu hadi 30% ya katikati ya QR Code kufunikwa na logo bila kuharibu uwezo wa kusomeka kwa simu.
❓ Je, QR Code zilizotengenezwa hapa zina muda wa kuisha (expiry date)? Hapana! QR Code tunazounda hapa ni Static QR Codes. Zinafanya kazi milele na hazina ada ya kila mwezi wala muda wa kuisha.
❓ Je, ni salama kuweka passwords za Wi-Fi ya ofisini kwangu? Ndiyo, ni salama 100%. Mfumo hautumi data yoyote kwenye server. QR Code inatengenezwa moja kwa moja kwenye browser ya simu au kompyuta yako.