Kila Picha Unayopiga na Simu Yako Inaonyesha Ulipo - Watu Wanaweza Kukufuatilia Nyumbani Kwako Kupitia Picha Tu Na Kuhatarisha Usalama Wako
Habari wadau,
Natumai mko poa
Nimekuwa nikifanya uchunguzi mdogo baada ya kuona watu wengi humu mtandaoni mna-post picha za magari mnayouza, nyumba mnazopangisha, na hata watoto wenu.
Je, mnajua kila picha mnayopiga na simu yenu ya mkononi inabeba siri 3 ndani yake bila ninyi kujua?
1. Mahali halisi mlipopiga picha (GPS Coordinates - hadi mlango wa nyumba yako)
2. Muda na tarehe kamili
3. Aina ya simu na kamera mliyotumia
Hii inaitwa EXIF Metadata. Mtu yeyote akipakua picha yako kutoka Facebook, WhatsApp Status (ukituma kama Document), au JF, anaweza kuingia kwenye tovuti moja tu na kuona ulikuwa wapi hasa ulipopiga hiyo picha.
Mfano wa hatari: Unapiga picha ya gari lako nyumbani kwako na ku-post JF "Gari linauzwa". Mtu akipakua hiyo picha anaweza kujua nyumba yako iko Mbezi, mtaa gani, kwa kutumia GPS iliyopo ndani ya picha hiyo.
Nini nilijifunza na suluhisho nililojenga:
Baada ya kuona hii, nimekuwa kwa wiki 3 nikijaribu kutengeneza zana ndogo inayofuta hizo taarifa zote kwa sekunde 1, bila kupunguza ubora wa picha.
Tofauti na zana nyingine za mtandaoni zinazopakia picha yako kwenye server zao (ambayo ni hatari zaidi), hii niliyojenga inafanya kazi tofauti:
Picha haipandi popote. Kila kitu kinafanyika ndani ya simu yako tu. Hata ukizima bando baada ya kufungua ukurasa, bado itafuta GPS. Tumetumia teknolojia ya HTML5 Canvas kwa usalama 100%.
Nimeijaribu kwa picha zangu mwenyewe - GPS yote inafutika na ubora unabaki kama ulivyo.
Kwa wanaotaka kujifunza na kujaribu kupima picha zao kama zina GPS, nimeiacha bure hapa: Tafuta Google "futa exif data gridpdf" au nenda moja kwa moja hapaa [https://www.gridpdf.com/image-tools/exif/].
Shauri: =>Kabla ya kupost picha yoyote ya nyumbani kwako, gari, au familia, pitisha hapa kwanza uhakikishe GPS imefutika.
Mnaonaje wadau, mlitarajia hii hatari au ulishawahi kuifahamu kabla?
_Imeandaliwa na: Eng. Suleiman Nassoro Ally- Kizumari Technologies
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)
*1. Je, Facebook na Instagram wanafuta EXIF wenyewe?*
Ndiyo wanafuta wakipost kawaida. LAKINI ukituma picha kama "Document" kwenye WhatsApp au uki-upload JF kama attachment, EXIF inabaki 100%. Ndio hatari kubwa.
*2. Je, nikifuta EXIF ubora wa picha unapungua?*
Hapana kabisa. Zana yetu ya GridPhoto inafuta taarifa za siri tu, sio picha yenyewe. Picha inabaki na ubora ule ule wa HD.
*3. Je, inafanya kazi bila bando?*
Ndiyo. Fungua ukurasa mara moja ukiwa na bando, kisha zima data. Bado utaweza kufuta EXIF kwa sababu kila kitu kinafanyika ndani ya browser ya simu yako.
Unahitaji kusimamia mafaili yako ya PDF sasa hivi?
Tumia Zana Zetu za Bure